Hours : Mon To Fri - 10AM - 04PM, Sunday Closed

News

Event Image

MTANANGE WA KISOKA: OOLA PRIMARY VS OOLA PRE-FORM ONE!

⚽ MTANANGE WA KISOKA: OOLA PRIMARY VS OOLA PRE-FORM ONE! 

​Hekaheka za michezo zilinoga pale Uwanja wa Mpira wa Shule ya Sekondari Manyara, ambapo wanafunzi wetu walionyesha burudani safi ya soka iliyojaa ushindani mkubwa, vipaji, na burudani isiyo na kifani! 

​Timu ya Wavulana (Oola Primary vs Oola Pre-Form One): Mchezo ulikuwa mkali na wa kasi sana kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho! Vijana wa Oola Primary walionyesha ubabe na kuibuka na ushindi mtamu wa magoli 2 kwa 1 dhidi ya Pre-Form One. 

​Timu ya Wasichana (Girls Match): Wasichana wa Pre-Form One hawakuacha nyuma! Waliwasha moto mkubwa uwanjani na kuibuka washindi kwa ushindi mnono wa magoli 6 kwa 4 kwenye mpambano uliokuwajaa shangwe na mbwembwe nyingi! 

​Tunatoa pongezi za dhati kwa timu zote mbili kwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu na mchezo safi wa kiungwana! Hivi ndivyo tunavyojenga afya, vipaji, na umoja kupitia michezo. 

​