Hours : Mon To Fri - 08AM - 06PM, Sunday Closed

News

Event Image

OOLA SCHOOL YAANDA IFTAR YA PAMOJA MWEZI MTUKUFU WA RAMADAN

Uongozi wa OOLA Academy School unapenda kuwashukuru kwa dhati wazazi, wanafunzi, viongozi wa dini, wawakilishi wa taasisi mbalimbali pamoja na waumini wote walioshiriki katika tukio la Futari ya Pamoja (Iftar) lililofanyika tarehe 15 Machi 2026 katika viwanja vya shule.

Tukio hili lilikuwa na mafanikio makubwa na lilienda sambamba na malengo yake ya kuwakutanisha wadau wa shule katika mazingira ya mshikamano, upendo na ushirikiano. Washiriki walipata fursa ya kufuturu pamoja, kubadilishana mawazo, na kuimarisha uhusiano kati ya shule na jamii inayotuzunguka.

Aidha, tukio hili lilikuwa sehemu ya kuthamini na kushiriki baraka za mwezi mtukufu wa Ramadhani, huku likisisitiza umuhimu wa umoja na kusaidiana katika jamii.

Uongozi wa shule unatoa shukrani za pekee kwa wote waliojitokeza na kuchangia kufanikisha tukio hili, ikiwa ni pamoja na wadau na wafadhili mbalimbali waliounga mkono juhudi hizi.

Tunatarajia kuendelea kushirikiana nanyi katika matukio yajayo kwa maendeleo ya wanafunzi wetu na jamii kwa ujumla.

Asanteni sana na Ramadhani njema.

OOLA Academy School

Recent News